Mazingira FM

Dr Nchimbi: Asilimia 90 ya wakazi wa Nyatwali wamelipwa

22 April 2025, 8:42 pm

Waliosalia asilimia 10 katika kipindi kifupi malipo yatakamilika huku akimuagiza waziri wa fedha kukamilisha mchakato huo ndani ya siku 14

Na Adelinus Banenwa

Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Taifa Dr Emmanuel Nchimbi amewatoa hofu wakazi wa kata ya Nyatwali ambao bado wanadai sehemu ya malipo yao kutokanana mpango wa serikali wa kuwahamisha wa kata hiyo

Mapokezi ya Dr Nchimbi Bunda

Dr Nchimbi amesema hayo wakati akisalimia wakazi wa Bunda katika mapokezi ya ziara yake mkoani Mara ambapo mbali na mambo mengine amelitaja suala la kata ya Nyatwali na madai ya wananchi waliosalia kuwa analifahamu.

Dr Nchimbi amesema kwa taarifa alizonazo wananchi zaidi ya asilimia 90 tayari wamelipwa na wameondoka na waliobaki asilimia 10 katika kipindi kifupi malipo yatakamilika huku akitumia hadhara hiyo kumuagiza waziri wa fedha Dr Mwiguru Nchemba kufanyia kazi malipo hayo ndani ya siku 14

Dr Emmanuel Nchimbi