Mazingira FM
Mazingira FM
19 April 2025, 8:28 pm

Sheria ya bima inayatambua makundi matatu ambayo ni taasisi inayotoa bima, taasisi, kampuni au mtu anayekata bima na kundi la tatu ni wanaopata majanaga ambao hawafungamani na makundi mawili ya awali
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa jamii kuondoa dhana ya kukata bima mara baada ya kupata majanga badala yake wakate bima mapema ili kuweka mazingira mazuri ya ulinzi wa vyombo vyao vya moto pamoja na mali.
Hayo yamesemwa na Abdulhakimu Habibu afisa kutoka shirika la bima la taifa NIC mkoani Mara tawila Musoma wakati akizungumza kupitia kipindi cha ufahamu wa sheria radio mazingira fm
Aidha habibu amesema katika sheria ya bima inayatambua makundi matatu ambayo ni taasisi inayotoa bima, taasisi, kampuni au mtu anayekata bima na kundi la tatu ni wanaopata majanaga ambao hawafungamani na makundi mawili ya awali