Mazingira FM

Diwani na wenzake wapandishwa kizimbani Bunda

5 April 2025, 12:08 am

Watuhumiwa hao wanatajwa kutenda makosa ya Matumizi mabaya ya Madaraka, kughushi nyaraka kwa lengo la kumdanganya muajiri, kuunda vikundi hewa na kufanya ubadhirifu wa shilingi milioni 3.

Na Adelinus Banenwa

Watu wanne akiwemo diwani wilayani Bunda wamefikishwa mahakani kwa tuhuma za kuunda vikundi hewa na kufanya ubadhirifu wa shilingi milioni 3.

Akisoma kesi hiyo namba 7441 ya mwaka 2025 mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Bunda Mhe Betron Sokanya, mwendesha mashtaka wa TAKUKURU amesema watuhumiwa Bonji William Bugeni afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya mji wa Bunda na Emmanuel Malibwa Diwani wa kata ya Nyamakokoto, Godfrey Zephania Merengo na Kharidi Deus Kabusure kwa nyakati tofauti walitenda makosa hayo.

Mwendesha mashtaka huyo amesema watuhumiwa hao wametenda makosa ya Matumizi mabaya ya Madaraka, kughushi nyaraka kwa lengo la kumdanganya muajiri, kuunda vikundi hewa na kufanya ubadhirifu wa shilingi milioni 3.

Washtakiwa wote wamekana mashtaka na wapo nje kwa dhamana huku kesi hiyo ikihairishwa hadi tarehe 2 May 2025 itakapotajwa tena .