

2 April 2025, 6:49 pm
Amewataadharisha viongozi hao kuepuka watu wanaotaka nafasi za uongozi kwa kutumia rushwa.
Na Adelinus Banenwa
Katibu wa Elimu, malezi na Maadili jumuiya ya wazazi CCM Bunda ndugu Masau Magala ameitaka jamii kuzingatia kuzingatia suala la Maadili na kuepuka vitendo vya ukatili kwa watoto ili kujenga jamii yenye heshima.
Masau ameyasema hayo leo April 2, 2025 katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya jumuiya ya wazazi CCM kata ya Bunda stoo ambapo mbali na mambo mengine pia Masau amewataadharisha viongozi hao kuepuka watu wanaotaka nafasi za uongozi kwa kutumia rushwa.
Naye diwani wa kata ya bunda stoo Mhe Flavian Chacha Nyamageko akielezea baadhi ya miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake amesema ni pamoja na upatikanaji wa shule mbili za sekondari, shule moja mpya ya msingi, hospitali ya halmashauri huduma ya maji safi kusogea karibu na wananchi pamoja na miradi mingine.
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM kata ya Bunda stoo ndugu Waryoba Kunzu amesema katika maadhimisho yao wamefanya shughuli mbalimbali ikiwemo kupanda miti eneo la ofisi za cha hicho kata ya Bunda stoo pamoja na kufanya usafi.
Aidha Kunzu amesema maelekezo yaliyotolewa na mgeni rasmi wameyachukua na kilichobaki ni kutafanyia kazi ikiwemo suala la ukatili pamoja na rushwa kuelekea Uchaguzi.