Mazingira FM

Wanafunzi Dr. Nchimbi sekondari wavutiwa na Mazingira FM

21 March 2025, 6:04 pm

Baadhi ya wanafunzi kidato cha nne Dr Nchimbi sekondari baada ya ziara yao kwenye studio za radio Mazingira Fm

Wameirai jamii kusikiliza na kutembelea kituo cha Radio Mazingira Fm kutokana na huduma bora za utangazaji na ufikisha wa mahudhui ya habari kwa wananchi na jamii kwa ujumla.

Na Adelinus Banenwa

Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne shule ya Sekondari Dr Nchimbi wavutiwa na mazingira ya studio za radio Mazingira Fm

Wanafunzi hao walifika studio za radio Mazingira Fm leo March 21, 2025 kwa lengo la kujifunza katika project ya kuona umuhimu wa mitandao ya kijamii kwenye vyombo vya habari .

Baadhi ya wanafunzi kidato cha nne Dr Nchimbi sekondari wakipata maelezo mafupi namna ya uendeshaji vipindi ndani ya studio za radio Mazingira fm

Katika ujumbe wao Mara baada ya ziara yao wamesema hawakutegema kupata ushirikiano walioupata kutoka kwa viongozi na wafanyakazi wa radio Mazingira Fm.

Aidha wameirai jamii kusikiliza na kutembelea kituo cha Radio Mazingira Fm kutokana na huduma bora za utangazaji na ufikisha wa mahudhui ya habari kwa wananchi na jamii kwa ujumla

Sauti za baadhi ya wanafunzi kidato cha nne Dr Nchimbi sekondari