

21 March 2025, 5:45 pm
Inadaiwa mama huyo aliyetambulika kwa jina la Neema Musimu John alichukua hatua ya kumuunguza mtoto huyo baada ya kujisaidia kwenye nguo bila kutoa taarifa.
Na Adelinus Banenwa
Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka mitano ambaye jina lake limehifadhiwa amekutwa ameunguzwa kwa moto kwenye kiganja cha mkono wa kulia na mtu anayedaiwa kuwa ni mama yake.
Tukio hilo la aina yake ambalo jamii na viongozi wa chama na serikali wameliita tukio la ukatili limegundulika leo March 21 2025 eneo la mtaa wa Mapinduzi kata ya Bunda mjini halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara.
Mwenyekiti wa mtaa wa Mapinduzi Daniel Yapanda amesema taarifa za tukio hilo amezipata majira ya saa tatu za asubuhi ambapo alipigiwa simu na wasamalia wema na alipofika alita mtoto huyo ana hali mbaya na kiganja hicho sehemu ambayo ameunguzwa ilikuwa imeanza kuoza kutokana na kukosa huduma ya afya kwa wakati
Yapanda ameongeza kuwa kutokana na hali hiyo aliwasiliana na mtenda, diwani wa kata pamoja na viongozi wa chama ngazi ya wilaya ambapo na wao walipofika waliafikiana mtoto huyo apelekwe Manyamanyama hospitali.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Bunda mjini Mzamili Ibrahim Kirwanila amesema tangu walipogundua tatizo hilo bado wanaendelea kushirikiana na mamlaka ya vyombo vya usalama kuhakikisha mzazi wa mtoto huyo anapatikana na anachukuliwa hatua.
Lucia John katibu jumuiya ya wazazi CCM Bunda amesema kama jumuiya inayohusika na suala la malezi wamelaani kitendo hicho kilichodaiwa kufanywa na Mama mzazi wa mtoto huyo huku akibainisha kuwa tayari kama jumuiya imehusika kuhakikisha mtoto huyo anapata matibabu pia chama kitahusika kuhakikisha wahusika walioshiriki wanachukuliwa hatua.
Inadaiwa mama huyo aliyetambulika kwa jina la Neema Musimu John inadaiwa alichukua hatua ya kumuunguza mtoto huyo baada ya kujisaidi kwenye nguo bila kutoa taarifa.
Jitihada za kulitafuta jeshi la polisi dawati la jinsia na watoto