

13 February 2025, 11:46 am
Halmashauri ya wilaya ya Bunda yatakiwa mwaka huu kwenye bajeti kutenge fedha kwa ajili ya kulipa madeni ya wadau mbalimbali.
By Edward Lucas.
Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dr Vicent Naano Anney amemwagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bunda mwaka huu kwenye bajeti watenge fedha kwa ajili ya kulipa madeni ya wadau mbalimbali
Amesema ni aibu kuona watu wanajitokeza mara kwa mara wakidai pesa zao katika halmashauri ambazo waliingia nazo mikataba na kutoa tahadhari kwa miradi mipya inayotekelezwa awamu hii kuingia katika madeni
Naano ameyasema hayo katika mkutano wa baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda lililofanyika jana tarehe 12 Feb 2025 kupokea taarifa ya robo ya pili ya mwaka wa fedha 2024/ 2025
Katika baraza hilo la madiwani likiongozwa na makamu mwenyekiti wa baraza, Mhe Keremba Irobi pamoja na mambo mengine lilipokea na kujadili taarifa ya TARURA, RUWASSA na Taarifa ya mthibiti ubora wa shule halmashauri ya wilaya ya Bunda.