Mazingira FM

Wanahabari wapigwa msasa uandishi bila kuleta taharuki

12 February 2025, 6:56 am

Ili kuwezesha jamii isipate madhara zaidi ni wajibu wa mwandishi wa habari na chombo cha habari kujua namna ya mbinu sahihi za kutumia ili kuleta matokeo chanya ambayo pia hayawezi kuleta taharuki kwenye jamii husika.

Na Adelinus Banenwa

Waandishi wa habari wa redio za kijamii wajengewa uwezo wa namna bora ya kuandika habari na kuandaa vipindi vya afya ambavyo haviwezi kusababisha taharuki kwa jamii ila kutoa elimu na uelewa.

Baadhi ya washiriki wa semina wakiendelea na mafunzo ya mbinu sahihi za uandaaji wa habari

Hayo yamejili leo Feb 11, 2025 ikiwa ni siku ya pili ya semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka redio za kijamii kanda ya ziwa kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Marburg chini ya Ufadhili wa Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto UNICEF

Prosper Laurent Kwigize mwandishi wa habari na mchambuzi wa masuala ya utatuzi wa migogoro moja kati ya watoa mada amesema ili kuwezesha jamii isipate madhara zaidi ni wajibu wa mwandishi wa habari na chombo cha habari kujua namna ya mbinu sahihi za kutumia ili kuleta matokeo chanya ambayo pia hayawezi kuleta taharuki kwenye jamii husika.

Washiriki wakiendelea kupata uzoefu wa uandaaji wa habari za afya

Ndugu proper amesema kuwa mara nyingi kwenye changamoto za magonjwa hasa ya milipuko yanapotokea watu wanataka kujua je vyombo vya habari vinasema nini hivyo ni wajibu wa chombo cha habari au mwanahabari mwenyewe kuseti ajenda ambayo kupitia maswali yake yanaweza kusaidia kutoa mwelekeo kwa jamii kuhusu ugonjwa husika.