

7 February 2025, 6:25 pm
NMB imetoa jumla ya madawati 200 yenye thamani ya shilingi milioni 20 katiak shule tatu za halmashauri ya wilaya ya Bunda.
Na Adelinus Banenwa
Katibu tawala wilaya ya Bunda Ndugu Salumu Mtelela ameishukuru benki ya NMB kwa misaada Mbalimbali wanayoitoa wilayani Bunda hasa katika Sekta ya elimu na Afya.
Mtelela ameyasema hayo leo Feb 7, 2025 wakati wa kupokea madawati 200 kutoka NMB shughuli iliyofanyika shule ya msingi Mwiruruma kata Iramba halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara.
Kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano katibu tawala huyo amesema sekta ya elimu inahitaji wadau wengi kushirikiana na serikali kuleta Maendeleo na NMB wamekuwa wadau kila wakati wakisaidia vifaa katiaka sekta ya elimu poamoja na afya.
Naye Faraja Ng’ingo meneja wa NMB kanda ya Ziwa amesema ni utaratibu wa banki ya NMB kama taasisi ya kifedha kurejesha faida kwa wananchi ambapo asilimia 1 ya faidi hurejeshwa kwa wananchi kupitia kutoa msaada wa vifaa katika sekta ya Afya, Elimu pamoja na majanga.
Faraja amebainisha kuwa baada ya kupokea maombi na kuyapitia benki hiyo ya NMB imetoa jumla ya madawati 200 yenye thamani ya shilingi milioni 20 katika shule ya msingi Mwiruruma madawati 100, shule ya msingi Buguma madawati 50 na shule ya msingi Mumagunga dawati 50 zote za halmashauri ya wilaya ya Bunda jambo la Mwibara
Kaimu afisa elimu msingi halmashauri ya wilaya ya Bunda Ndugu phinias Ouko ameishukuru bank ya NMB kwa msaada huo huku akibainisha kuwa kwa madawati 100 yaliyotolewa shule ya msingi Mwiruruma yamemaliza kabisa upungufu wa madawati shuleni hapo na kuifanya shule hiyo wanafunzi wote kukaa kwenye madawati.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mwiruruma Maliselina Tarimo amesema kabla ya msaada huo wa NMB wanafunzi takribani 300 walikuwa wanakaa chini hivyo ujio wa madawati hayo 100 umewafanya wanafunzi wote wa shule yake wawe na mahali pa kukaa.
Naye Dr Masinde Bwire miongoni mwa wadau wa maendeleo kwa halmashauri ya wilaya ya Bunda ameishukuru banki ya NMB huku akitoa wito kwa wakazi wa Mwiruruma kuwa na tabia ya kujitokeza kwa wingi pale wadau wanapofika kwenye maeneo yao kuwasaidia shughuli za maendeleo kwa kuwa wingi wao unaongeza chachu kwa wadau hao kusaidia zaidi.