

6 February 2025, 8:29 pm
Wananchi watakiwa kulinda miradi ili iweze kudumu na kuhudumia kizazi cha sasa na hata kile kijacho
Na Adelinus Banenwa
Kiasi cha shilingi milioni 88 kimeshatumika kati ya shilingi milioni 100 kwenye ujenzi wa Nyumba ya walimu shule ya sekondari Bunda mjini mkoani Mara
Mkuu wa shule ya sekondari ya Bunda mjini amesema nyumba hiyo imejengwa katika mfumo wa Nyumba mbili ndani ya moja ambayo familia mbili za walimu wataishi pindi itakapokamilika.
Ufafanuzi huu umetolewa kwa kamati ya fedha ya halmashauri ya mji wa Bunda iliyofika shuleni hapo kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo wa nyumba ya mwalimu.
Katika ujumbe wake mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bunda na diwani wa kata ya Sazira Mhe Michael Kweka mbali na kupongeza mkuu wa shule kwa usimamizi mzuri wa mradi amemtaka kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ili nyumba hiyo iweze kutumika.
Kwa upande wake mkurugenzi wa mji wa Bunda Juma Haji ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wailinda miundombinu inayoletwa na serikali katika maeneo yao ili iendelee kuhudumia kizazi cha sasa na hata kijacho.