Mazingira FM

Dc Bunda awakutanisha wafanyabiashara kujadili changamoto zao

28 January 2025, 6:39 am

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano

Lengo la mkutano wake na wafanyabiashara ni kukaa na kujadili namna gani ya kushirikiana ili kusonga mbele kwa mwaka huu wa 2025.

Na Edward Lucas

Wafanyabiashara wilayani Bunda wajadili changamoto zao katika sekta ya mifugo, uvuvi , kilimo pamoja na uuzaji bidhaa.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dr Vincent Naano Anney amesema lengo la mkutano wake na wafanyabiashara ni kukaa na kujadili namna gani ya kushirikiana ili kusonga mbele kwa mwaka huu wa 2025 na kufanya kazi zao kwa weledi

Baadhi ya washiriki kwenye mkutano wa wafanyabiashara Bunda

Dr. Naano amesema wafanyabiasha wilaya ya Bunda wamekuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya wilaya kupitia kodi zao hivyo kuna umuhimu wa kukaa na kujadili changamoto zinazowakabili ili kutafuta ufumbuzi kwa pamoja.

Baadhi ya washiriki kwenye mkutano wa wafanyabiashara Bunda

Dr Naano ameyasema hayo leo wakati akizungumza na radio Mazingira Fm

Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Malaika mjini Bunda ambapo kwa upande wake aliwakilishwa na Katibu Tawala Wilaya ya Bunda ndugu Salumu Mtelela.

Katibu Tawala wilaya ya Bunda Ndugu Salumu Mtelela akizungumza katika mkutano wa wafanyabiashara Bunda

Sambamba na hilo DC Naano amesema zaidi ya Bil 13 zipo wilaya ya Bunda kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo

Amesema uwepo wa fedha hizo ni fursa kwa wafanyabiashara kwa kutoa huduma mbalimbali wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali kama ujenzi wa shule na miradi ya maji