Mahakama ya Bunda yazindua maadhimisho wiki ya sheria
25 January 2025, 8:02 pm
Miongoni mwa maeneo yatakayokuwa yanalengwa zaidi katika wiki hii ya sheria ni pamoja na migogoro ya ardhi, mirathi, ndoa na talaka miongoni mwa maeneo mengine.
Na Adelinus Banenwa
Mahakama ya wilaya ya bunda imezindua rasmi leo wiki ya sheria inayoongozwa na kauli mbiu isemayo ”Tanzania ya 2050 nafasi ya taasisi inayosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya dira ya taifa ya maendeleo”
Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Bunda mulokozi kamuntu amesema katika wiki hii ya sheria mahakama kwa kushirikiana na mawakili na wadau wengine watatoa elimu na msaada wa kisheria kwa makundi mbalimbali bila malipo.
Kamuntu ameongeza kuwa miongoni mwa maeneo yatakayokuwa yanalengwa zaidi katika wiki hii ya sheria ni pamoja na migogoro ya ardhi, mirathi, ndoa na talaka miongoni mwa maeneo mengine.
Leonard Magwayega kwa niaba ya chama cha mawakili Tanganyika TLS amesema wiki hii ni muhimu kwa wananchi wote hasa wenye changamoto za kisheria ambapo watapewa msaada awa kisheria na mawakili bila gharama yoyote katika kipindi cha siku saba .
Magwayega ameongeza kuwa miongoni mwa huduma watakazozitoa kuwa ni pamoja na kuwaandikia wateja wao nyaraka mbalimbali za kisheria pamoja na kuwajibia baadhi ya nyaraka ambazo hawazielewi bila gharama.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mhe mkuu wa wilaya ya Bunda Dk Vicent Naano amewahimiza wqananchi wote wilayani bunda kutumia fursa hiyo ya wiki ya sheria kufika katiak maeneo yaliyoainishwa ili kupata ufumbuzi wa changamoto zao.