Mazingira FM

NMB yakabidhi vifaa vya ujenzi vya milioni 10 kwa shule za Salama A na B, Bunda

24 January 2025, 6:37 pm

Viongozi wa NMB wakikabidhi kwa viongozi wa shule sehemu ya bati walizotoa msaada kwa shule za Salama A na B

“NMB kama wadau wa maendeleo wanajikita sana katika kusaidia sekta ya elimu ambapo husaidia madawati na vifaa vingine, afya husaidia kwenye vitanda pamoja na vifaa vingine vya kusaidia matibabu, pia husaidia kwenye majanga yanayoipata nchi.”

Na Adelinus Banenwa

Benki ya NMB imekabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 10, kwa shule za msingi Salama A na Salama B.kufuatia madhara yaliyosababishwa na mvua iliyokuwa imeambatana na upepo mkali ulioikumba kata ya Salama, Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Mvua hiyo ilitokea tarehe 29 Agosti 2024 majira ya saa 12 jioni na kusababisha uharibifu mkubwa wa madarasa matatu pamoja na nyumba za walimu katika shule za msingi Salama A na Salama B.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Humphrey Daniel Kaaya meneja mahusianao banki ya NMB Kanda ya ziwa  amesema wao kama wadau wa maendeleo wametoa mabati 72 kila shule mbao pamoja na misumari ambavyo jumla yake vinathamani ya shilingi 10 milioni hii ikiwa ni sehemu ya kurejesha faida kwa wateja wao.

Sauti ya Humphrey Daniel Kaaya meneja mahusianao banki ya NMB Kanda ya ziwa
Viongozi wa NMB wakikabidhi kwa viongozi wa shule sehemu ya misumari waliyotoa msaada kwa shule za Salama A na B

Humphrey ameongeza kuwa wao kama wadau wa maendeleo wanajikita sana katika kusaidia sekta ya elimu ambapo husaidia madawati na vifaa vingine, afya husaidia kwenye vitanda pamoja na vifaa vingine vya kusaidia matibabu, pia husaidia kwenye majanga yanayoipata nchi.

Sauti ya Humphrey Daniel Kaaya meneja mahusianao banki ya NMB Kanda ya ziwa

 Kwa upande wao wazazi na wanafunzi wameshukuru msaada uliotolewa na banki hiyo huku wakiiomba serikali kusaidia kukarabati majengo ya shule hizo za salama A na B ili kujenga mazingira bora ya wanafunzi kujifunza na kufundishia.

Sauti za wazazi
Viongozi wa NMB wakikabidhi kwa viongozi wa shule sehemu ya mbao walizotoa msaada kwa shule za Salama A na B

Deusdedit Bimbalirwa, mkuu wa divishen ya elimu ya awali na msingi Bunda DC,  Kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dr Vicent Naano mbali na kuishukuru benki ya NMB kwa msaada wao katika miradi ya mandeleo hasa katika sekta ya elimu afya na majanga pia amesema msaada huo utapunguza changamoto ya vyumba vya madarasa hali inayopelekea watoto kusoma kwa zamu ikiwa wengine wanaingia asubuhi na wengine wanaingia jioni.

Sauti ya Deusdedit Bimbalirwa, mkuu wa divishen ya elimu ya awali na msingi Bunda DC,

Aidha Bimbalirwa  amewataka wazazi na walezikuhakikisha wanawapele watoto shule na kuhakikisha wanawanunulia mahitaji yote ya shule ikiwa ni pamoja na sare, daftari pia kuchangia chakula cha wanafunzi shuleni ili watoto hao waweze kusoma bila changamoto.

Sauti ya Deusdedit Bimbalirwa, mkuu wa divishen ya elimu ya awali na msingi Bunda DC,