Mazingira FM

UWT Bunda yazindua maadhimisho miaka 48 ya CCM

24 January 2025, 6:03 pm

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bunda Ndugu Abraham Mayaya Magese, Akipanda mti kama ishara ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 48 ya CCM kwa UWT Bunda

UWT Bunda mwaka huu wamepanga kufanya shughuli mbalimbali za kijamii katika kuelekea sherehe hizo za miaka 48 ya CCM ambazo ni pamoja na kupanda miti walau 50 kila kata, kufanya usafi katika ofisi za umma, kutembelea makundi ya watu wasiyojiweza pamoja na kufanya mikutano.

Na Adelinus Banenwa

Jumuiya ya wanawake chama cha mapinduzi wilaya ya Bunda UWT wamezindua maadhimisho ya miaka 48 ya chama hicho kwa kupanda miti ofisi za CCM wilaya ya Bunda.

Akizungumza katika uzinduzi huo katibu wa UWT wilaya ya Bunda Evodia Zumba amesema kwa utaratibu wa chama kuelekea maadhimisho ya siku ya kuanzishwa kwa chama hicho mara nyingi huwa zinatangulia jumuiya kuadhimisha sherehe hizo.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bunda Ndugu Abraham Mayaya Magese, akikabidhi mti kwa moja ya viongozi wa UWT kata ikiwa ni ishara uzinduzi wa maadhimisho ya CCM kwa UWT Bunda

Zumba amefafanua kuwa kwa upande wa UWT Bunda mwaka huu wamepanga kufanya shughuli mbalimbali za kijamii katika kuelekea sherehe hizo za miaka 48 ya CCM ambazo ni pamoja na kupanda miti walau 50 kila kata, kufanya usafi katika ofisi za umma, kutembelea makundi ya watu wasiyojiweza pamoja na kufanya mikutano ya kuwashukuru wananchi kwa kukiamini chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliyofanyika Mwezi Nov mwaka jana.

Sauti ya katibu wa UWT wilaya ya Bunda Evodia Zumba
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Bunda Ndugu Merysiana Sabuni. akipanda mti ikiwa ni ikiwa ni ishara uzinduzi wa maadhimisho ya CCM kwa UWT Bunda

Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT wilaya ya Bunda Ndugu Merysiana Sabuni amesema wao kama jumuiya wamejipanga kuhakikisha wanaadhimisha miaka 48 ya CCM kwa kufanya shughuli hizo za kijamii.

Sauti ya mwenyekiti wa UWT wilaya ya Bunda Ndugu Merysiana Sabuni

Naye mgeni rasmi katika uzinduzi huo ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bunda Ndugu Abraham Mayaya Magese ameipongeza jumuiya ya UWT kwa uamuzi wao wa kuzindua maadhimisho hayo kwa kufanya mambo hayo manne ambayo yanakusa moja kwa moja ilani ya chama ya mwaka 2020 na 2025

Sauti ya mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bunda Ndugu Abraham Mayaya Magese