Mazingira FM

Ubovu wa barabara wasababisha ujenzi wa shule kusuasua Mihingo

10 January 2025, 10:59 am

Mradi wa shule msingi mpya ya inayojengwa katiaka kijiji cha Mekomariro kata ya Mihingo

Wasimamizi na mafundi kuwa mbali na eneo la mradi, ushiriki mdogo wa wananchi,  ubovu wa  barabara kati ya Mekomariro  senta hadi kitongoji cha Nyansirori, chanzo cha kusuasua kwa ujenzi wa shule mpya ya msingi.

Na Mariam Mramba

Imeelezwa kuwa ushiriki mdogo wa wananchi,  ubovu wa  barabara kati ya Mekomariro  senta hadi kitongoji cha Nyansirori, chanzo cha kusuasua kwa ujenzi wa shule mpya ya msingi katika eneo hilo.

Hayo yameelezwa na wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge wa jimbo la Bunda  Mhe Boniphace  Getere  alipofika  kusikiliza kero za wananchi katika kata ya Mihingo kijiji cha Mekomariro Jan 8, 2025

Aidha wananchi hao pia wamedai mradi huo umekuwa ukisuasua kutokana na wasimamizi na mafundi kuwa mbali na eneo la mradi.

Sauti za wananchi sababu za kusuasua kwa mradi
Mwenyekiti wa kijiji cha mekomariro Juma Msanya

Mwenyekiti wa kijiji cha mekomariro Juma Msanya amewataka  wananchi wa kijiji hicho washirikiane kufanya kazi na wazabuni waliochukua kazi hiyo wapeleke viashiria kwa wakati pamoja na wasimamizi wa mradi huo wakae karibu na eneo la mradi.

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji cha mekomariro Juma Msanya

Naye mbunge wa jimbo la Bunda Boniphace Getere ameitaka  ofisi ya mkurugenzi kuteua msimamizi atakae kuwa eneo la kazi muda wote ili kusaidia mradi kwenda kwa haraka huku  amewakemea baadhi ya wananchi wanaokwamisha shughuli za maendeleo.

sauti ya mbunge wa jimbo la Bunda Boniphace Getere