Zaidi ya milion 584.2 kujenga shule ya Amali Mugeta
8 January 2025, 7:03 pm
Milioni 584.2 zimetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Amali katika kijiji cha Manchimweru
Na Mariam Mramba
Zaidi ya shilingi milioni 584.2 zimetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Amali katika kijiji cha Manchimweru kata ya Mugeta katika halimashuuri ya wilaya Bunda mkoani Mara.
Hayo yameelezwa na afisa elimu sekondari halamshauri y awilaya ya Bunda Bi.Nambua January 7/ 2027 alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa wananchi kwenye ziara ya mbunge wa jimbo la Bunda Mhe Boniphas Getere wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya kata hiyo.
Naye kaimu mkurugenzi wa halmashuri ya wilaya ya Bunda Stapha Nashoni amewataka wananchi hao kuthamini miradi inayoletwa na serikali katika maeneo yao huku akihaidi kuwa serikali itaendelea kutatua changamoto zinazo wakabili ikiwemo kuanzisha mnada katika eneo hilo.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Bunda Boniphace Mwita Getere amewataka wananchi wa kijiji cha Mwanchimweru kushiriki nguvu kazi zao katika kutekeleza mradi huo kwa kushirikiana na viongozi serikali ya kijiji huku akiwataka wakandarasi kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.