Mazingira FM

Kambarage Wasira akabidhi viti 100 kwa jumuiya ya wazazi CCM Bunda

31 December 2024, 7:45 pm

Mwenyekiti wa kamati ya fedha na mipango chama cha mapunduzi wilaya ya Bunda Ndugu Kambarage Masatu Wasira kushoto akikabidhi viti 100 kwa mwenyekiti wa jumiya ya wazazi CCM Bunda Adv Leonard Magwayega

“Changamoto ya ukata ndani ya jumuiya ya wazazi ndiyo imepelekea kubuniwa mradi wa kiuchumi kusaidia jumuiya hii kujiendesha” Lucy John

Na Adelinus Banenwa

Mwenyekiti wa kamati ya fedha na mipango chama cha mapunduzi wilaya ya Bunda Ndugu Kambarage Masatu Wasira amekabidhi viti 100 kwa jumiya ya wazazi CCM

Ndugu Kambarage amekabidhi viti hivyo kwenye baraza la wazazi chama cha mapinduzi lililofanyika leo DEC 31, 2024 alipoalikwa kuwa mgeni rasmi.

Mwenyekiti wa kamati ya fedha na mipango chama cha mapunduzi wilaya ya Bunda Ndugu Kambarage Masatu Wasira

Ndugu Kambarage amesema kitendo cha jumuiya kubuni miradi yao ni jambo la kupongezwa hasa ukizingatia jumuiya hizo zinao wadau mbalimbali wa kuwashika mkono katika kuanzisha miradi hiyo ambapo yeye binafsi baada ya kupokea maombi yao ametoa viti hivyo 100 ikiwa ni sehemu ya kuwaunga mkono

Aidha amezirai jumuiya zingine kuiga mfano wa jumuiya ya wazazi kuanzisha miradi itakayowasaidia.

Sauti ya Mwenyekiti wa kamati ya fedha na mipango chama cha mapunduzi wilaya ya Bunda Ndugu Kambarage Masatu Wasira
Mwenyekiti wa jumiya ya wazazi CCM Bunda Adv Leonard Magwayega

Mwenyekiti wa jumiya ya wazazi CCM Bunda Adv Leonard Magwayega amesema wakati mwingine jumuiya hiyo inakosa heshma na viongozi wake kuonekana kuwa ombaomba kutokana na kuhitaji msaada wa kuijenga na kuisaidia jumuiya hiyo hali inayopelekea viongozi hao wakati mwingine kutumia fedha zao za mifukoni kuendesha shughuli za jumuiya.

Sauti ya Mwenyekiti wa jumiya ya wazazi CCM Bunda Adv Leonard Magwayega
katibu wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Bunda Ndugu Lucy John

Naye katibu wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Bunda Ndugu Lucy John amesema wazo la uanzishwaji wa mradi liliwajia kupitia maoni ya kamati ya utekelezaji ya jumuiya hiyo baada ya kukithiri kwa ukata ndani ya jumuiya hiyo hasa ukizingatia haina kiongozi yeyote amayeweza kuwashika mkono ikiwa ni pamoja na mbunge wala Diwani.

Lucy ameongeza kuwa walipendekeza kuwepo kwa mradi wa viti ambapo hadi sasa wamefikisha viti 204 na lengo lao ni kufikisha viti 1000

Lucy amemshukuru Ndugu Kambarage Masatu Wasira kwa mchango wake huo wa viti 100 ambapo amesema kupitia mradi huo utapunguza kuombaomba.

Sauti ya katibu wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Bunda Ndugu Lucy John
Baadhi ya wajumbe wa baraza la wazazi CCM Bunda

Nao baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wamesema wanautegemea sana mradi huo kutokana na changamoto zilizokuwa zikiwapata ikiwemo kukosa hata fedha ya nauli kwenda kwenye vikao wilayani.

Sauti za baadhi ya wajumbe wa baraza la wazazi CCM Bunda