Mbunge Maboto Mradi wa TACTIC kuwa neema Bunda
7 December 2024, 10:48 pm
Mradi wa uendelezaji miji TACTICS kwa mji wa Bunda utakapoanza utasaidia barabara nyinyi za bunda mjini Kupata lami.
Na Adelinus Banenwa
Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto amesema mradi wa uendelezaji miji TACTICS kwa mji wa Bunda utakapoanza utasaidia barabara nyinyi za bunda mjini Kupata lami.
Mhe Maboto ameyasema hayo Dec 6 2024 katika kamati ya ushauri ya wilaya ya Bunda DCC ambapo amesema miradi mingi imetekelezwa kwa kiwango kikubwa katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya sita kama vile miradi ya maji, elimu, umeme barabara pamoja huduma za Afya.
Mhe Maboto amesema kwa sasa jimbo la Bunda mjini mradi mkubwa unaosubiriwa ni mradi wa uendelezaji miji wa TACTIC ambapo ukishaanza kutekelezwa utasaidia kwa kiasi kikubwa kuufanya mji wa Bunda kuwa wa kisasa na kwa maelezo ya waziri alitaja mradi huo kutekelezwa December mwaka huu.