Mazingira FM

Wapiga kura Bunda mjini walalamika majina kutoonekana vizuri

27 November 2024, 5:23 pm

Baadhi ya wananchi wakitafuta majina yao kabra ya kupiga kura

“Utaratibu ni mzuri ila changamoto kubwa ni majina hayaonekani vizuri hayajapangwa kwa kufuata mtililiko wa herufi”

Na Adelinus Banenwa

Wananchi walioteremka vituoni lei kupiga kura kutimiza haki yao ya msingi ya kuwachagua viongozi wa serikali za mtaa katika eneo la halmashauri ya mji wa Bunda wamelalamikia majina yaliyobandikwa kutoonekana vizuri

wananchi wakiwa wamepanga foleni kwa ajili ya kupiga kura

Wakizungumza na redio Mazingira fm ilipotembelea baadhi ya vituo katika baadhi ya mitaa ya Bunda mjini wananchi hao wamesema utaratibu wa upigaji wa kura uliyowekwa ni mzuri lakini changamoto ni majina kutoonekana vizuri ( yanaonekana kwa kufifia).

Wamesema hali hiyo inasababisha wananchi kuchukua muda mrefu kuangalia majina

moja ya wapiga kura akitafuta jina lake kabla ya kupiga kura

“Utaratibu ni mzuri ila changamoto kubwa ni majina hayaonekani vizuri hayajapangwa kwa kufuata mtililiko wa herufi na mvua imenyesha imeyanyeshea hivyo ni babu sana kuyaona” amesema mmoja wa wananchi ambaye hakutaka jina lake litajwe.

sauti za baadhi ya wananchi baada ya kupiga kura Bunda