TAKUKURU Mara yawaonya wagombea watoa rushwa
23 November 2024, 6:05 pm
Baadhi ya matendo ambayo yakifanyika inatafsiri kuwa ni rushwa ni pamoja na ugawaji wa tisheti, kanga, shati, chumvi, sabuni sukari au sherehe kabla wakati na baada ya uchaguzi.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa wananchi kutoa taarifa za vitendo vya rushwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyiaka 27 nov 2024.
Wito huo umetolewa na Winfrida Kanyika afisa TAKUKURU mkoa wa Mara alipokuwa akizungumza kupitia radio Mazingira Fm ndani ya kipindi cha Ufahamu wa Sheria ambapo amesema jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa si la TAKUKURU pekee bali kwa wananchi wote.
Winfrida asema iwe ni chama cha siasa au mgombea hatakiwi kushawishi watu kuwapigia kura kwa kutumia rushwa huku akitaja baadhi ya matendo ambayo yakifanyika inatafsiri kuwa ni rushwa ni pamoja na ugawaji wa tisheti, kanga, shati, chumvi, sabuni sukari au sherehe kabla wakati na baada ya uchaguzi.
Winfrida ameongeza kuwa katika kipindi hiki cha uchaguzi baadhi ya wananchi wamekuwa wakiwashawishi wagombea kutoa rushwa jambo ambalo ni kinyume na sheria.