Mazingira FM

BUWSSA watambulisha mradi wa bilioni 1.6 kata ya Wariku

30 October 2024, 10:15 am

Mkurugenzi wa BUWSSA Bi Esther Giryoma, Picha na Adelinus Banenwa

Mradi huu ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuhudumia wakazi elfu 33 pia unatarajiwa kujengwa ndani ya miezi mitano hadi kukamilika.

Na Adelinus Banenwa

Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Bunda BUWSSA chini ya mkurugenzi Bi Esther Giryoma imetangaza mradi wa maji wa bilioni 1.6 kwa wakazi wa kata ya wariku halmashauri ya mji wa Bunda.

wakazi wa kata ya Wariku walipojitokeza kupokea mradi wa maji kutoka BUWSSA, Picha na Adelinus Banenwa

Akizungumza wakati wa utambulishaji wa mradi huo mkurugenzi wa BUWSSA Bi Esther Giryoma amesema mradi huo utakuwa na Components mbalimbali ikiwemo uchimbaji wa mitaro na ulazaji mabomba kilometa 40 ujenzi wa tenki lenje ujazo wa cubic meter 200,000 pamoja na uwepo wa vituo sita au zaidi vya uchototaji maji kwa wananchi.

Sauti ya mkurugenzi wa BUWSSA Bi Esther Giryoma
Mkurugenzi wa BUWSSA Bi Esther Giryoma, Picha na Adelinus Banenwa

Aidha mkurugenzi huyo wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na waziri wa maji mhe Jumaa Aweso kwa kukubali and andiko na kuamua wakazi wa Kata ya Wariku wapate maji huku akiwataka wananchi kuhakikisha miradi inayoletwa kwenye maeneo yao wanailinda kwa wivu mkubwa ili iendelee kuwahudumia wao na vizazi vijavyo.

Sauti ya mkurugenzi wa BUWSSA Bi Esther Giryoma
wakazi wa kata ya Wariku walipojitokeza kupokea mradi wa maji kutoka BUWSSA, Picha na Adelinus Banenwa

Kwa upando wao wakazi wa kata ya Wariku wakiongozwa na diwani wa kata hiyo Mhe Kalulu Foda Manyonyi wameishukuru serikali ya Mhe Rais Samia pamoja na Mamlaka ya maji Bunda BUWSSA kwa kuwakumbuka na kuwafikishia mradi huo ambao utakapokamilika utawawezesha wakazi hao kuondokana na changamoto ya maji ambayo imewasumbua kwa muda mrefu hasa akina mama.

Sauti ya wakazi wa Wariku