Mazingira FM

Waliomaliza kulipwa Nyatwali wahimizwa kuondoka

16 October 2024, 5:04 pm

Mkuu wa mkuu wa mkoa wa Mara Kanal Evans Mtambi mwenye miwani akizungumza kwenye eneo la ulipaji fidia kwa wakazi wa Nyatwali, Picha na Adelinus Banenwa

Mkuu wa mkoa ametoa rai kwa wakazi wa Nyatwali ambao tayari wameshapokea hundi zao kuhakikisha wanafanya hima kuondoka katika maeneo hayo

Na Adelinus Banenwa

Imeelezwa kuwa serikali inakwenda kuhitimisha zoezi la ulipaji fidia kwa wakazi wote wa Nyatwali waliotathminiwa katika mitaa yote minne ya kata ambayo ni Kariakoo, Serengeti, Tamau pamoja na Nyatwali.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la ulipaji fidia mkuu wa mkoa wa Mara Kanal Evans Mtambi amesema kiasi cha shilingi bilioni 45.99 kilichotolewa na serikali kulipa fidia zoezi linaelekea ukongoni huku akiwashukuru wananchi kwa mwitikio mzuri wa zoezi hilo.

Mkuu wa mkuu wa mkoa wa Mara Kanal Evans Mtambi mwenye miwani akizungumza kwenye eneo la ulipaji fidia kwa wakazi wa Nyatwali, Picha na Adelinus Banenwa

Aidha Mhe Mtambi amemshukuru rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kutoa fedha hizo ili kuwaepusha wakazi wa Nyatwali na adha waliyokuwa wakiipata ya wanyama waaribifu wakiwemo tembo na wanyama wengineo.

Baadhi ya makundi ya Tembo yakionekana kusogea eneo la Nyatwali, Picha na Adelinus Banenwa

Mbali na shukrani hizo pia mkuu wa mkoa ametoa rai kwa wakazi wa Nyatwali ambao tayari wameshapokea hundi zao kuhakikisha wanafanya hima kuondoka katika maeneo hayo kwa kuwa tayari yameanza kushuhudiwa makundi makubwa ya tembo katika maeneo mbalimbali ndani ya kata hiyo hali inayoashiria hatari kwa watu watakaoendelea kubaki.

Mkuu wa mkuu wa mkoa wa Mara Kanal Evans Mtambi mwenye miwani akizungumza kwenye eneo la ulipaji fidia kwa wakazi wa Nyatwali, Picha na Adelinus Banenwa

Sambamba na hilo Mhe Mtambi amekemea tabia za baadhi ya makampuni ya ukopeshaji ambayo hayazingatii utaratibu wa riba na kutumia mwanya huo kuwadhurumu wananchi wanaoondoka Nyatwali ambapo amemuagiza mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano kusimamia hilo ili kila mwananchi anapata haki yake kwa mujibu wa sheria ya mikopo ya benki kuu.

Baadhi ya wakazi wakiwa katika maandalizi ya kuondoka Nyatwali baada ya kupata fidia, Picha na Adelinus Banenwa

Ikumbukwe tangu adhma ya serikali kutangaza kulitwaa eneo la kata ya Nyatwali maarufu kama Guba ya speak na mchakato wake wa tangu tarehe 22 mwezi Dec 2022 na tarehe 5 mwezi Sept 2024 uzinduzi wa ulipaji fidia ulizinduliwa rasmi ambapo lengo kuu ni kuunganisha eneo la Nyatwali na hifadhi ya taifa ya Serengeti ili kulinda ikolojia ya wanyama hii ikiwa ni kwamujibu wa Kamishna msaidizi mwandamizi wa uhifadhi Stephano Msumi ambaye ni mkuu wa hifadhi ya taifa ya Serengeti.