Mazingira FM

Zaidi ya milion 700 zatumika miradi ya maendeleo Sazira

9 October 2024, 8:36 am

Diwani wa kata ya Sazira na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bunda Michael Kweka

Katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan miradi iliyotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa zahanati mpya tatu, vyumba vya madarasa vya kutosha shule ya sekondari sazira, mradi wa maji wa Misisi Zanzibar pamoja na barabara za mitaa

Na Adelinus Banenwa

Diwani wa kata ya Sazira na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bunda Michael Kweka ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka miradi mingi ya maendeleo katika kata hiyo.

Diwani huyo ameyasema hayo alipotembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa katika kata hiyo,

Mhe Kweka amesema ndani ya kata ya Sazira katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan miradi iliyotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa zahanati mpya tatu, vyumba vya madarasa vya kutosha shule ya sekondari sazira, mradi wa maji wa Misisi Zanzibar, barabara za mitaa miongoni mwa miradi mingine.

Sauti ya Diwani wa kata ya Sazira na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bunda Michael Kweka

Aidha mhe kweka amewataka wananchi kujitokeza katika zoezi la uandikishaji daftari la makaazi kuanzia tarehe 11 oct hadi tarehe 20 oct 2024 ambalo litatumika kupiga kura za wenyeviti katika uchaguzi serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika 27 nov 2024