Mazingira FM

Vijiji 389 Bunda DC kushiriki uchaguzi serikali za mitaa

27 September 2024, 1:20 pm

Msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya wilaya ya Bunda George Stanley Mbilinyi, Picha na Adelinus Banenwa

Kwa mujibu wa kifungu cha 57 cha sheria ya serikali za mitaa sura ya 287 na kifungu cha 16 cha serikali za mitaa sura 288 uchaguzi  kufanyika kila baada ya miaka 5.

Na Adelinus Banenwa

JUMLA  ya vitongoji 389 ,vijiji  78 na kata 19 za halmashauri ya wilaya ya Bunda zinatarajia kushiriki katika  uchaguzi wa serikali za mitaa  unaotarajiwa kufanyika , November 27 2024.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika katika ukumbi  wa Halmashauri ya Wilaya ya BUNDA ,msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya wilaya ya Bunda George Stanley Mbilinyi amesema kwa mujibu wa kifungu cha 57 cha sheria ya serikali za mitaa sura ya 287 na kifungu cha 16 cha serikali za mitaa sura 288 uchaguzi  kufanyika kila baada ya miaka 5.

Baadhi ya washiriki kwenye kikao cha msimamizi wa uchaguzi kutoa maelekezo kuelekea uchaguzi serikali za mitaa Bunda DC, Picha na Adelinus Banenwa

Aidha Mbilinyi ametaja viongozi wenye sifa za kushiriki katika uchaguzi  pamoja na nafasi za uongozi zinazogombewa kuwa ni pamoja na wenyeviti serikali za Vijiji, Vitongoji na wajumbe wa maeneo hayo.

Sauti ya George Mbilinyi

Mbilinyi amesema zoezi la uandikisha daftari la makazi litafanyika kati ya tarehe 11 October hadi 20  October 2024, pia zoezi la uchukuaji wa fomu kwa wagombea litakuwa kati ya tarehe 1- 7 November 2024 na pia   na muda wa kampeini ni siku saba  ambazo ni kati ya tarehe 20 hadi 26 November 2024.

Sauti ya George Mbilinyi.
moja ya wadau wa uchaguzi akichangia kwenye kiikao cha cha msimamizi wa uchaguzi kutoa maelekezo kuelekea uchaguzi serikali za mitaa Bunda DC, Picha na Adelinus Banenwa

Sambamba na hayo pia Mbilinyi amewataka viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wazee maarufu pamoja na wadau wengine wote kushirikiana kutoa elimu kwa wananchi kujitokeza katika kujiandikisha.

Mkutano huo umehudhuriwa na watendaji wa kata ,watendaji wa vijiiji,viongozi wa siasa ,viongozi wa dini,  pamoja na wakuu wa idara wote kutoka halmashauri ya  wilaya ya Bunda.