Mazingira FM

FRI-SUCODE yaitaka jamii kuchukua hatua dhidi ya fistula

19 September 2024, 8:52 pm

Nakaniwa Mshana, mratibu wa mradi wa FRI-SUCODE, Picha na Adelinus Banenwa

dalili kwa mama mwenye fistula ya uzazi ambapo ni pamoja na kutokwa na aja ndogo au kubwa kwa mfululizo bila kuwa na uwezo wa kujizuia, kutokwa na harufu mbaya ya mkojo au kinyesi miongoni mwa dalili zingine.

Na Adelinus Banenwa

Imeelezwa kuwa kutohudhuria kliniki kipindi cha ujauzito kwa wanawake, kukaa na uchungu kwa muda mrefu na uzazi pingamizi  ni moja ya visabashi vya fistula ya uzazi kwa wanawake.

Hayo yamesemwa na Nakaniwa Mshana, mratibu wa mradi wa FRI-SUCODE  kutoka shirika la Fistula Faundation inayoshughulika na utoaji elimu na kuwasaidia wanawake wenye changamoto ya fistula kwenye jamii.

Amesema wanawaweke wengi wanaopata fistula ya uzazi mara nyingi ni wale wanaokuwa wanakosa muda mzuri wa maandalizi wakati wa kwenda kujifungua huku wengine wakiwa na dhana kwamba wanasubiri kuivisha uchungu.

Sauti ya Nakaniwa Mshana, mratibu wa mradi wa FRI-SUCODE

Nikanawa ameongeza kuwa zipo dalili kwa mama mwenye fistula ya uzazi ambapo ni pamoja na kutokwa na aja ndogo au kubwa kwa mfululizo bila kuwa na uwezo wa kujizuia, kutokwa na harufu mbaya ya mkojo au kinyesi miongoni mwa dalili zingine.

Sauti ya Nakaniwa Mshana, mratibu wa mradi wa FRI-SUCODE
Immaculata Cornel afisa miradi wa FRI-SUCODE, Picha na Adelinus Banenwa

Kwa upande wake Immaculata Cornel afisa miradi wa FRI-SUCODE amesema hali ya fistula ya uzazi kwa wanawake inatibika na matibabu yake ni bure kupitia shirika la Fistula Faundation  kupitia mradi wa FRI-SUCODE ambapo katika kipindi chote cha matibabu mama atapata huduma zote bure ikiwemo chakula nauli ya kwenda hospitali na kurudi miongoni mwa huduma zingine’

Sauti ya Immaculata Cornel afisa miradi wa FRI-SUCODE

Akitaja namna ya kupata msaada wa matibabu Nakaniwa Mshana amesema mtu yeyote mwenye ndugu ambaye ana changamoto ya fistula ni kupitia mawasiliano ambayo ni 0787537743 na 0756692922.