Mazingira FM

Ajali nyingine yaua na kujeruhi waombolezaji Bunda

29 August 2024, 6:28 pm

Gari lililopata ajali eneo la Sanzate

Watu watatu wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika Kijiji cha Sanzate wilayani Bunda Mkoa wa Mara.

Na Adelinus Banenwa

Watu watatu wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika Kijiji cha Sanzate wilayani Bunda Mkoa wa Mara.

Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Hiace iliyokuwa imebeba waombolezaji kutokea Mausoma kuelekea Mugeta kwa ajili ya maziko 

Akizungumza na mazingira fm kwa njia ya simu, Diwani kata ya Nyamuswa Ibrahim Mganga Igai amesema ajali hiyo imetokea Agosti 28,2024 saa 9 alasiri nay eye alipata taari za ajali hiyo kupitia vijana wake alikuwa amewatuma mugeta kikazi.

Aidha diwani Ibrahimu amesema baada ya kupokea taarifa hizo aliwasiliana na mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha Ikizu na Mugeta ambao walitoa gari za kubebea wagonjwa yaani ambulence ili kuwawahisha majeruhi hospitali.

sauti ya Diwani kata ya Nyamuswa Ibrahim Mganga Igai

Kwa upande wake mganga wa zamu kituo cha afya ikizu dkt Ally Abdallah Nasoro ameiambia mazingira fm kuwa kituo hicho kilipokea wangonjwa (majeruhi) 12 n ammoja kati yao alifariki dunia wakati akipatiwa huduma za awali na wengine watano walipewa rufaa kwenda hospitali za mbele na wagonjwa wengine sita wameendelea kupata huduma kituoni hapo na hali zao zinaendelea vizuri

Sauti ya Dkt Ally Abdallah Nasoro,

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Salim Morcase amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, ambapo amesema waombolezaji hao walikuwa wakielekea katika kijiji cha Mugeta wilayani Bunda kwa ajili ya mazishi.

Amesema ajali hiyo imetokea baada ya tairi la mbele la kushoto kupasuka kwa pamoja na tairi la nyuma hivyo gari kukosa mwelekeo.