Mazingira FM

Utani wa Bodaboda, mmoja apoteza maisha kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali Bunda

29 August 2024, 10:42 am

Abdullah Halfani John dereva pikipiki aliyepoteza maisha kwa madai ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali na dereva mwenzake

Utani wa bodaboda vijiweni ulivyopelekea kifo cha mwenzao mmoja baada ya kuchomwa na kitu che ncha kali kifuani.

Na Adelinus Banenwa

Dereva pikipiki (bodaboda) aliyetambulika kwa jina la Abdullah Halfani John (41) amepoteza maisha akidaiwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali na dereva mwenzake.

Kwa mujibu wa mashuhuda wameiambia Mazingira Fm kuwa tukio hilo limetokea tarehe 28 Aug 2024 jion ambapo inadaiwa Abdullah alishambuliwa na mwenzake aliyejulikana kwa jina la Baraka na kitu chenye ncha kali eneo la kifuani upande kushoto baada ya kutokuelewana baina yao.

sauti za mashuhuda

Kwa upande  wake mwenyekiti wa waendesha pikipiki kituoni hapo ameiambia mazingira fm kuwa tukio hilo limewashtua sana na nilakustaajabisha kutokana na mazingira yake pia kwa masuala yote ya utani uliopitiliza umeshapigwa marufuku kituon hapo.

Sauti ya mwenyekiti wa bodaboda Nyasura

Hadija Amiri mke wa marehemu amesema majira ya jioni alishangaa kuona shemeji zake wakifika nyumbani wakimuulizia mwenye nyumba alivyohoji wanamuhitaji wa nini ndipo walipomueleza kuwa Abdallah amefariki kwa ajali.

Sauti ya mke wa marehemu

Abdallah ambaye ni dereva pikipiki kituo cha mabasi ya Mwanza eneo la Nyasura, Bunda mjini ameacha mke na watoto watatu.