Mazingira FM

Viongozi watakiwa kutoa taarifa kwa wananchi kuepusha upotoshaji

28 August 2024, 1:46 pm

Mwenyekiti wa CCM wa kata ya Nyasura  ndugu Marco Mabula, Picha na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa viongozi kutoa taarifa sahihi na kwa wakata kwa wananchi ili kuepuka migogoro na kusambaa kwa taarifa za upotoshaji.

Na Adelinus Banenwa

Kamati ya siasa kata ya Nyasura ikiongozwa na mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo ndugu Marco Mabula imewaagiza viongozi wa kata na mitaa ya kata hiyo kutoa taarifa sahihi za Miradi na shughuli nyingine za serikali  kwa  wananchi ili kuepukana na taarifa za upotoshaji zinazosambazwa na watu wasiyokuwa waaminifu.

Baadhi ya wajumbe kwenye kikao cha kamati ya siasa yakata ya Nyasura, Picha na Adelinus Banenwa

Hayo yamesema na mwenyekiti wa CCM wa kata ya Nyasura  ndugu Marco Mabula katika kikao cha kamati ya siasa ya kata hiyo na wajumbe wa kamati ya maendeleo ya kata kilichoketi kwa lengo la kupokea taarifa mbalimbali.

Afisa mtendaji wa kata ya Nyasura Jerrymary Kamugisha, Picha na Adelinus Banenwa

Afisa mtendaji wa kata ya Nyasura Jerrymary Kamugisha amesema kamati ya siasa ilikuwa na mambo matatu ya kufahamu kutoka kwa kamati ya maendeleo ya kata kutokana na wananchi kutokuwa na ufahamu wa mambo hayo ikiwa ni pamoja na Kiongozi wa mbio za mwenge kukataa kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalumu, Shule ya sekondari ya Dkt Nchimbi kushindwa kupokea wanafunzi wa kidato cha nne na taarifa kuwa fedha zilikuwa zimeletwa kwa ajili ya ujenzi wa sekondari mpya kwenye kata hiyo kuwa zimehamishwa.

Diwani wa kata ya Nyasura Mhe Magigi Samweli Kiboko, Picha na Adelinus Banenwa

Naye diwani wa kata ya Nyasura Mhe Magigi Samweli Kiboko amesema lengo kuu viongozi ni kuhakikisha wanafanya kazi ya wananchi na kuhakikisha miradi inaletwa kwenye maeneo ya huku akitoa wito kwa wananchi kutafuta taarifa sahihi kutoka kwa viongozi ambayo majibu hayo yanapatikana kupitia mikutano ya hadhara na ofisi za kata na mitaa.

Kwa upande wao wajumbe wa kikao hicho wametaja kuridhika na majibu ya waalamu wa katika hoja tatu zilizohitaji majibu huku wakiendelea kuhimiza viongozi kuwa na utamaduni kutoa taarifa sahihi kwa wakati kwenye jamii ili kuondoa kusambaa taarifa za uongo na upotoshaji kwenye jamii.