Mazingira FM

Vitambulisho 528 vya NIDA vyakwama ofisi ya mtendaji Bunda mjini

23 August 2024, 2:10 pm

Kagoye Mwenge, mtendaji kata ya Bunda mjini, Picha na Adelinus Banenwa

Wananchi watakiwa kuepuka kutoa namba zao za NIDA ovyo ili kuepuka changamoto ya kutumika vibaya kwa namba hizo.

Na Gaudensia Zakayo

Jumla ya vitambulisho 528 vya taifa (NIDA) havijachukuliwa katika kata ya Bunda mjini.

Hayo yamesemwa na Mtendaji wa kata ya Bunda Mjini Kagoye Mwenge wakati akizungumza na redio Mazingira Fm ofisini kwake ambapo amesema jumla ya vitambulisho vilivyopokelewa ofisi ya mtendaji ni 6628 hadi sasa vitambulisho 6589 vishachukuliwa na vitambulisho 39 wenye navyo imebainika wamefariki.

Aidha, amewasihi wananchi kutoa taarifa kwa wale ambao wamehama wilaya ya Bunda kuja kuchukua kitambulisho cha taifa.

Sauti ya Kagoye Mwenge

Sambamba na hayo pia Bi Kagoye amewatahadharisha wananchi kuwa wanatakiwa kuwa makini na vyanzo vya taarifa vinavyohusisha matumizi ya kitambulisho cha taifa.