Mazingira FM

Aliyeuawa na wasiyojulikana azikwa Bunda

6 August 2024, 1:18 pm

Baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mama Dina Kabula aliyeuawa baada ya kushambuliwa na watu wasiyojulikana akiwa nyumbani kwake, Picha na Adelinus Banenwa

Waombolezaji walaani kitendo cha mtu kuvamiwa ndani kwake kisha kuuawa wameliomba jeshi la polisi kuwasaka wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria

Na Adelinus Banenwa

Mwanamke aliyeuawa baada ya kushambuliwa na watu wasiyojulikana nyumbani kwake katika mtaa wa Rubana kata ya Balili mjini Bunda azikwa

Akizungumza na waombolezaji katika shughuli ya mazishi ya mama huyo aliyetambulika kwa jina la DINA Kabula Mbilize, mchungaji wa kanisa la FPCT Bunda mchungaji Omoso amesema familia haitakiwi kuwaza habari za visasi badala yake waviachie vyombo vya sheria kufanya kazi yake

Mbali na hilo pia mchungaji Omoso amewataka waombolezaji na wananchi kuendelea kuwatia moyo wanafamilia hasa katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza ndugu yao hasa wale walioshuhudia tukio la kushambuliwa kwa ndugu yao.

sauti ya mchungaji Omoso

Mwenyekiti wa mtaa wa Rubana MALASE KILANGI amewataka wakazi wa mtaa wake kutoa taarifa za uharifu na waharifu, hasa kama kuna mtu ana taarifa zozote zinazoweza kulisaidia jeshi la polisi kwenye uchunguzi wa tukio hilo basi asisite kutoa taarifa hizo,

Malaseamesema mtu mwenye taarifa za siri za tukio hilo anaweza kuwaona viongozi wa mtaa, kata kwa maana ya mtendaji au kupeleka taarifa hizo kwa jeshi la polisi.

SAUTI YA MWENYEKITI

Kwa upande wake diwani wa kata ya Balili Mhe Thomas Tamka amesema tukio hilo mbali na kusikitisha pia limeacha pengo kwenye familia na kwa upande wake ameliomba jeshi la polisi kuwasaka wahusika na kuwachukulia hatua kali za kisheria

Aidha Mhe Tamka ameiomba familia kuendelea kuwa watulivu na kuwa na moyo wa subra wakata serikali ikiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Sauti ya Diwani

Ikumbukwe kwa mujibu wa mume wa marehemu MALENYA MADUHU SUBHA tukio la kushambuliwa kwa DINA Kabula Mbilize ambaye kwa sasa ni marehemu lilitokea usiku wa tarehe 2 Augost 2024 akiwa nyumbani kwake amekaa na wanafamilia wengine, ndipo inadaiwa walitokea watu watatu na kumshambulia kisha kutoweka kusikojulikana bila kuchukua kitu kingine chochote pia bila kujeruhi mtu mwingine yeyote.