Mnzava akubali kuweka jiwe la msingi mradi wa maji taka Bunda
3 August 2024, 8:28 pm
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2024 Ndg. Godfrey Eliakim Mnzava amepongeza Mamlaka ya Maji Bunda BUWSSA kufuata utaratibu wa manunuzi serikalini yaani mfumo wa NEST utekelezaji mradi wa maji taka Butakale.
Na Adelinus Banenwa
Mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2024 umeweka jiwe la msingi katika mradi wa maji taka unaosimamia na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Bunda BUWSSA.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo wa maji taka, mkurugenzi wa BUWSSA Bi Esther Giryoma amesema mradi huo unagharimu zaidi ya shilingi bilion1.728.
Mbali na hayo, mradi pia utahusisha ujenzi wa tanuru kwa ajili kuteketeza taka ngumu,barabara ya kilomita (Km) 2.5 ya changarawe,nyumba ya mlinzi, uzio wa kulinda miundombinu, ununuzi wa magari mawili ya kukusanyia maji taka yenye ujazo wa lita 10,000 na 5,000 na kuweka umeme eneo hilo. Hadi sasa utekelezaji umefikia asilimia 35 na Mkandarasi yuko eneo la kazi na kazi inaendelea.
Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2024 Ndugu Godfrey Eliakim Mnzava amesema amelidhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi pia ameipongeza mamlaka ya maji Bunda BUWSSA kufuata utaratibu wa manunuzi serkalini yaani mfumo wa NEST hivyo amekubali kuweka jiwe la msingi leo tarehe 3 AUG 2024.