Mazingira FM

Mlinzi akutwa ameuawa na wanaodaiwa ni majambazi akiwa lindoni

31 July 2024, 8:04 am

Mwanaume mmoja ambaye ni mlinzi akutwa ameuawa katika eneo lake la lindo wezi waondoka na tv na vinywaji

Na Adelinus Banenwa

Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Baraka Juma 38 mkazi wa mtaa wa mapinduzi kata ya Bunda mjini ammmmmm ni mlinzi wa kampuni ya Bunda Security amekutwa ameuawa usiku wa kuamkia tarehe 30 July eneo lake la lindo.

Mlinzi huyo aliyekuwa analinda kwenye baa ya CN mjini Bunda

Kwa mujibu wa wenye lindo hilo wamesema wamebaini mlinzi huyo kuwa ameuawa baada ya kuamka asubuhi kukuta sehemu ya bidhaa za baa zimeibiwa kwenye kaunta huku mlinzi akiwa chini na akiwa na majeraha sehemu ya kichwani ndipo walipowasiliana na viongozi wa kampuni yake na Jeshi la polisi.

sauti za mashuhuda kwenye lindo

Mohamedi Makongoro ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Bunda Security amesema taarifa za Baraka kushambuliwa eneo lake la lindo amezipata kutoka kwa Ps wake na kama kampuni wamesikitika sana na tukio hilo la kulaaniwa kwa mlinzi wao kuuawa

sauti ya mkurugenzi wa Bunda Security

Mohamedi Makongoro ameongeza kuwa kama kampuni wamepoteza mtu muhimu na kilichopo ni klushirikiana na familia kuhakikisha wanamuhifadhi salama baraka

Kwa upande wa ndugu wa Baraka wakizungumza na Mazingira Fm wamesema wanaiomba serkali kuwatafuta wahusika wa tukio hilo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

sauti za ndugu wa Baraka

James makoye ambaye ni kaka wa marehemu Baraka amesema, baraka ameacha mke na mtoto mmoja na kama familia wamepokea taarifa hizo kwa masikitiko.