BUWSSA yaendelea kutanua mtandao wa maji Bunda
30 July 2024, 9:44 am
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Bunda BUWSSA Bi, Ester Giryoma awewataka wananchi kufuata utaratibu wa maunganisho mapya ya maji ili kuepuka vishoka wanaoweza kuwaibia fedha zao
Na Mariam Mramba
Wananchi wa kata ya Bunda stoo, halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara wanaelekea kuondokana na changamoto ya ukosefu wa maji iliyokuwa inawakabiri kwa muda mrefu baada ya mamlaka ya maji Bunda BUWSSA kuanza kutandaza mabomba ya maji kwenye maeneo yao.
Hayo yamesemwa na wananchi wa kata hiyo hii leo kwenye kikao cha kukabidhi mabomba kilichoambana na zoezi la usambazaji na ulazaji mabomba katika mitaa minne ya Kata hiyo ambayo ni Kilimani,Miembeni,Idara ya maji na mtaa wa Butakale
Wakizungumza wakati wa zoezi hilo wenyeviti wa mitaa hiyo wamekiri kuwepo kwa changamoto ya maji kwa muda mrefu ambapo wamempongeza diwani wa kata ya Bunda stoo kwa jitihada alizofanya ili kuhakikisha wananchi wa maeneo hayo wanapata maji.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Bunda stoo Flavian Chacha Nyamageko amesema kuwa wahanga wakubwa wa changamoto hiyo walikuwa ni wanawakewaliokuwa wanatembea umbali mrefu kutafuta maji ambapo amewataka wananchi kutohujumu miundombinu hiyo ya maji badala yake waitunze
Naye Mkurugenzi wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Bunda BUWSSA Bi, Ester Giryoma amewatahadharisha wananchi hao kuepukana na vishoka ambao watataka kuwaunganishia maji kwa njia ya udanganyifu kwani malipo yote ya serikali yanalipwa kwa namba maalumu ya malipo (control number) na kutumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi kutunza miradi na kuitumia kwa uadalifu, kulipa bili kwa wakati pamoja na kutoa taarifa kwa yeyote atakayejihusisha na vitendo vya wizi wa maji.