Mazingira FM

Mama ajifungua mapacha walioungana, serikali yaingilia kati kusaidia kuwatenganisha

29 July 2024, 11:28 am

Rupa Memorial hospital sehemu ambayo mama amejifungua watoto mapacha walioungana. Picha na Adelinus Banenwa

Mama ajifungua mapacha walioungana mjini Bunda serikali yaingilia kati kusaidia kuwatenganisha

Na Adelinus Banenwa

Ni mama mmoja mkazi wa Bunda jina limehifadhiwa katika hali isiyiyo ya kawaida amejifungua watoto mapacha walioungana.

Kaimu mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Bunda Dkt Yusuph Wambura amesema mwanamke huyo amejifungua watoto mapacha walioungana na baada ya kupata taarifa hiyo alifika kituo cha kutolea huduma ambapo mama huyo alijifungulia ili kuona namna halmashauri inaweza kumsaidia.

Dkt Yusuph amesema suala hilo ni la kisayansi na lisihusishwe na imani za kishirikina huku akiongeza kuwa kama serikali tayari imetoa gari (ambulance) ili kuwasafirisha mama na watoto hao hospital ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya hatua zaidi za kitabibu.

Sauti ya Dkt Yusuph Wambura Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Bunda

Dkt Yusuph ametoa wito kwa mama wajawazito kwenda vituo vya kutolea huduma za afya na kupima kipimo cha ultrasound ambacho huangalia ukuaji wa mtoto tumboni pia wanawake wajawazito kuhakikisha wanajifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya.

Sauti ya Dkt Yusuph Wambura Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Bunda

Kwa upande wake katibu tawala wilaya ya Bunda Ndugu Salumu Mtelera amesema serikali wilayani Bunda inawapongenza madaktari wa hospitali ya Rupa Memorial kwa kumsaidia mama huyo kujifungua salama tena kwa njia ya kawaida bila upasuaji.

Katibu tawala wilaya ya Bunda Ndugu Salumu Mtelera,

Amewahakikishia wanafamilia kwamba serikali wilayani Bunda kuwa popote watakapopata changamoto wakiwa Bugando ili kuhakikisha wanapata huduma kwa wakati.

Sauti ya katibu tawala wilaya ya Bunda