Viongozi wa mitaa na kata fanyeni mikutano kufafanua miradi kwa wananchi
17 July 2024, 8:31 pm
Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto amewataka viongozi ngazi ya kata na mitaa kufafanua miradi inatoletwa na serikali katika maeneo yao kwa kuwa ni haki yao kuijua.
Na Adelinus Banenwa
Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto amewataka viongozi ngazi ya kata na mitaa kufafanua miradi inatoletwa na serikali katika maeneo yao kwa kuwa ni haki yao kuijua.
Mhe Maboto amesema hayo katika mwendelezo wa ziara yake kwenye mitaa ndani ya jimbo la Bunda mjini ambapo kwa siku ya leo amefanya mikutano ya hadhara katika mitaa ya Kisangwa, Chamgongo na mtaa wa Nyamatoke yote ikiwa ndani ya kata ya Mcharo.
Mikutano hiyo ya Mhe Robert Chacha Maboto inalenga kusikiliza kero za wananchi na kutatua changamoto zao pia kutoa mrejesho baada ya vikao vya bunge vilivyomalizika mwezi uliopita.
Akizungumzia suala la ushilikishwaji wananchi kwenye miradi Mhe mbunge maboto amesema mwananchi kujua mradi unaotekelezwa kwenye eneo lake na unathamani kiasi gani siyo jambo la hiari bali ni wajubu wa viongozi kufanya hivyo.
Kwa upande wao wakazi wa kata ya Mcharo kwa ujumla katika mitaa yote aliyoitembelea Mhe Maboto wamesema changamoto kubwa waliyonayo ni suala la ukosefu wa Maji safi na salama, barabara pamoja na umeme.