Wazazi wamlilia mbunge adhabu kwa wanafunzi wasiyopeleka chakula shuleni
15 July 2024, 9:00 pm
Titizo la ukosefu wa walimu wa sayansi na adhabu kwa wanafunzi ambao wazai wao wanashindwa kupeleka chakula shuleni vyatawala mkutano wa mbunge wa Bunda mjini katika kata ya Sazira.
Naa Adelinus Banenwa
Wakazi wa kata ya sazira mtaa wa ligamba wamelalamikia wanafunzi kuchapwa viboko pindi wazazi wanaposhindwa kupeleka mahindi na maharage shuleni.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara wa mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto katika kata ya Sazira wananchi hao wamesema kumekuwa na changamoto kubwa katika suala la uchangiaji chakula shuleni na walimu wamekuwa wakiwaadhibu watoto pindi mzazi asipotoa mahindi shuleni hali inayopelekea wanafunzi kuwa watoro kwa kuogopa adhabu.
Akito ufafanuzi katika mkutano huo diwani wa kata ya Sazira na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bunda Mhe Michael Kweka amesema hakuna sheria yoyote inayomruhusu mwalimu kutoa adhabu kwa mwanafunzi kutokana na mzazi kushindwa kupeleka chakula shuleni.
Amewataka wananchi kutoa taarifa kwake ikitokea mwalimu yeyote ndani ya halmashauri ya mji wa Bunda atatoa adhabu kwa mwanafunzi kutokana na mzazi kutopeleka chakula shuleni kwa sababu hilo siyo kosa la mwanafunzi.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Bunda mjini amewaomba wakazi wa jimbo la bunda mjini kujitahidi kuchangia chakula shuleni kwa kuwa itawasaidia watoto kujifunza vizuri bila njaa.