Nyaburundu sasa kupata shule mpya ya sekondari
13 July 2024, 9:27 am
Kiasi cha shilingi milion 584 zimetolewa na serikali kujenga shule mpya ya sekondari katika kijiji cha Nyaburundu ambayo itasaidia wanafunzi kutoacha shule.
Na Mariam Mramba
Jumla ya shilingi milioni mia tano themanini na nne zimetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Nyaburundu katika kijiji cha Nyaburundu, kata ya Ketare wilaya ya Bunda.
Hayo yamesemwa na Diwani wa kata hiyo Mhe Mramba Simba Nyamkinda alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji hicho kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika hii leo kijijini hapo.
Diwani Mramba amesema kuwa wamepitia changamoto nyingi ilikupatikana kwa shule ya Nyaburundu na kutumia nafasi hiyo kumpongeza mwenyekiti wa kijiji kwa jitihada alizizionesha ili kijiji hicho kipate shule ya sekondari.
Mwenyekiti wa kijii cha Nyaburundu Ndugu Hamis Said Madolo amewashuru diwani, mbunge na serikali kwa ujujenzi mla kwa jitihada walizozionesha katika jambo hilo na kwamba Nyaburundu ilikuwa kisiwani na sasa wametoka huko.
Kwa upande wao wananchi wa kijiji hicho wamewapongeza viongozi kwa kusikia kilio chao na kushirikiana kwapamoja ili kuhakikisha shule inapatikana ambapo wamesema wao ndio wanatakiwa kuwa kipaumbele kwa kuchangia nguvu zao ili kuhakikisha ujenzi wa shule hiyo unakamilika kwa wakati.