Maboto: Wananchi chagueni viongozi waadilifu serikali za mitaa
12 July 2024, 12:16 pm
Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto amewataka wananchi kuchagua viongozi waadilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao watakaowaletea Maendeleo
Na Adelinus Banenwa
Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto amewataka wananchi kuchagua viongozi waadilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao watakaowaletea Maendeleo.
Mhe Maboto ameyasema hayo leo July 11, 2024 katika siku ya kwanza ya ziara yake katika jimbo la Bunda mjini ambayo ameifanya katika kata ya Wariku kwenye mitaa ya Kiwasi, Manyago na Kangetutya ambapo amefanya mikutano ya hadhara na kuongea na wananchi.
Katika ziara hiyo Mhe mbunge Maboto akiwa ameambatana na diwani wa kata ya Wariku Mhe Kalulu Foda Manyonyi amesema wao kama wawakilishi wa wananchi kwa kushirikiana na serikali wanayo mambo makuu matano mahususi.
Mhe Maboto ametaja maeneo hayo kuwa ni Elimu, Afya , Maji, Barabara, Umeme na masuala ya Majanga.
Katika mikutano ya hadhara wananchi wamemshukuru mhe mbunge kwa jitihada anazozifanya kuwaletea Maendeleo.
Aidha wananchi hao wamesema ukosefu wa barabara za uhakika maji na umeme inapelekea kuchelewa kuinuka kiuchumi.
Naye Diwani wa kata ya Wariku Mhe Kalulu Foda Manyonyi amesema yeye kwa kushirikiana na Mbunge hadi sasa kata ya Wariku imepata zaidi ya shilingi Bilion 1.3 ambazo zimeenda kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa kituo cha Afya Wariku.
Mhe Maboto katika ziara hiyo amewahakikishia wananchi kuendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha changamoto zote za wananchi zinapungua kama siyo kuisha kabisa