Mazingira FM

Bulaya: Nyatwali haiwezekani walipwe fidia Tsh 490 kwa mita ya mraba wakati wako mjini

3 July 2024, 9:18 pm

Bunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA Mhe Esther Amos Bulaya, Picha na Edward Lucas

“Haiwezekani watu kutaabika kwa miaka miwili baada ya tathmini hawajalipwa lakini tathmini yenyewe kidogo shilingi 490 kwa mita ya mraba hapana lazima sisi kama viongozi tulisimamie hili” Esther Bulaya.

Na Adelinus Banenwa

Akizungumzia suala la Nyatwali Bunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA Mhe Esther Amos Bulaya amesema kwa mambo ambayo hakuweza kukubaliana nayo  ni wakazi wa Nyatwali kufanyiwa tathmini ya shilingi 490 kwa mita ya mraba angali hakuna kiwanja kinapatikana kwa bei hiyo ndani ya halmashauri ya mji wa Bunda.

Amesema kwa upande wa serikali wanalojukumu la kuhakikisha wanawalipa wakazi wa Nyatwali stahiki zao.

Bulaya amesema mara kadhaa amewapokea wakazi wa Nyatwali Dodoma na kuwakutanisha na viongozi mbalimbali wa serikali kupata suluhisho la eneo la Nyatwali 

Aidha Mhe Bulaya amesema kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya Tanzania inasema ukimfanyia mtu tathmini baada ya miezi sita bila kumlipa ni lazima umlipe na riba huku akiwataka wakazi wa Nyatwali kutokubali malipo bila riba wakati na wao kama viongozi wa wananchi wataendelea kulisimamia hilo hadi hatua ya mwisho.

Sauti ya Mhe Esther Bulaya