Mazingira FM

Bunda DC yapongezwa kwa kupata hati safi 2022/2023

27 June 2024, 12:35 pm

Mkuu wa mkoa wa Mara Kanal Evans Mtambi, Picha na Adelinus Banenwa

Mkuu wa mkoa aipongeza Bunda DC kwa kupata hati safi ya ukaguzi aielekeza menejimenti kufanyia kazi hoja za ukaguzi.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa mkoa wa Mara Kanal Evans Mtambi ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Bunda kwa kupata hati safi ya ukaguzi wa CAG.

Kanal Mtambi ameyasema hayo kwenye kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda kilichoketi 26 Juni 2024 kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali CAG kwa mwaka 2022 na 2023 ambapo halmashauri ya wilaya ya Bunda ilipata hati safi.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Mara Kanal Evans Mtambi
Baadhi ya madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda katika kikao cha kupitia hoja za ukaguzi riport ya CAG. Picha na Adelinus Banenwa

Katika maelekezo yake mhe Kanal Mtambi amesisitiza menejimenti ya halmashauri kuhakikisha inafanyia kazi hoja zote za mkaguzi ili hoja hizo ziweze kufungwa.

Aidha Kanal Mtambi ameelekeza kuchukuliwa hatua watumishi wote waliosababisha kwa makusudi hoja hizo za ukaguzi.