Mazingira FM

Mtoto aliyeokotwa saa chache baada ya kuzaliwa apewa jina la Jasmine

23 June 2024, 10:29 pm

Mtoto akiwiwa anaendelea kupata huduma kituo cha afya Bunda, Picha na Adelinus Banenwa

Mtoto aliyeokotwa saa chache baada ya kuzaliwa apewa jina la Jasmine na mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Bunda.

Na Adelinus Banenwa

Mtoto aliyetupwa saa chache baada ya kuzaliwa na kuokotwa na wasamalia apewa jina la Jasmine na mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Bunda.

Juma Haji mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Bunda leo alifika kituo cha afya Bunda anapoendelea kupatiwa huduma za kitabibu na ustawi mtoto huyo  kwa minajili ya kumuona na kisha kumpatia jina hilo la Jasmine.

Aidha radio Mazingira FM imezungumza na afisa ustawi wa jamii halamshauri ya mji wa Bunda Bi Frolence Dibogo ambaye amesema hadi sasa mama wa mtoto huyo hajatambulika huku akifafanua kuwa idara ya ustawi wa jamii inafanya utaratibu wa kupitia maombi ya watu waliojitokeza kutaka kumlea mtoto huyo na wengine wanataka kumuasili.

Amesema zipo taratibu za kufuata pindi unapotaka kumuasili mtoto ambapo ni pamoja na kujilidhisha kweli una uhitaji wa mtoto.

Dibogo amesema kama halmashauri na idara ya ustawi hawatoi kibali cha kuasili mtoto bali kibali hicho kinatolewa na kamishna wa ustawi wa jamii kwa mujibu wa sheria ya mtoto.

sauti ya Frolence Dibogo