Mazingira FM

DC Naano atoa siku 11 wakandarasi kumaliza barabara Bunda

19 June 2024, 6:01 pm

DC Naano akimsikiliza moja ya mkandarasi anayelima barabara za Bunda mjini, Picha na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda atoa siku 11 kwa wakandarasi wanaolima barabara Bunda mjini wawe wamemaliza asema kwa sasa hakuna kisingizio cha mvua.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Anney Naano ametoa siku 11 kwa wakandarasi waliopewa kazi za kutengeneza barabara ndani ya halamashauri ya Bunda mjini wawe wamemaliza.

Agizo hilo amelitoa leo June 19, 2024, baada ya kufanya ziara ya kukagua hali ya barabara ndani ya halmashauri ya mji wa Bunda katika kata za Nyasura, Bunda mjini na baadhi ya  maeneo ya kata ya  Bunda stoo.

DC Naano akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya usalama wiliya na viongozi kutoka ofisi ya TARURA wilaya ya Bunda, Picha na Adelinus Banenwa.

DC Naano amesema kuna dalili za baadhi ya wakandarasi wazembe ambao mwanzo walitaja hali ya mvua kuwakwamisha lakini hata baada ya mvua kuisha bado mwendo wao hauridhishi kutokana na barabara zilivyo.

Sauti ya DC Dkt Vicent Naano

Aidha amewataka wananchi kushiriki katika kulinda na kuitunza miundombinu inayopelekwa kwenye maeneo yao ambapo amesema katika baadhi ya maeneo wananchi wameng’oa vibao vya TARURA na  kwenda kuuza vyuma chakavu pia wanatoboa mambomba ili wapate maji ya bure jambo ambalo si la busara.

DC Naano akiwa ameshikilia mti baada ya kumaliza kuzima moto uliokuwa ukiwaka mlima boma, Picha na Adelinus Banenwa

Katika hatua nyingine DC Naano amepiga marufuku wananchi kuchanja kuni ( kusenya) kwenye maeneo ya milima inayozunguka ofisi ya mkuu wa wilaya ( bomani) kwa kuwa milima hiyo inahifadhiwa.

Ameagiza pia idara ya utunzaji wa misitu yaani TFS kuweka vibao vya matangazo vitakavyoainisha kuwa maeneo hayo hatakiwi mtu yeyote kuingia

Sehemu ya mlima liyochomwa moto na mtu asiyejulikana, Picha na Adelinus Banenwa

DC Naano amesema kumekuwepo na kasumba ya watoto kuchoma moto milima hiyo jambo ambalo lina hatarisha makazi ya wananchi wanaoishi karibu na milima hiyo huku akitoa onyo kwa yeyote atakayekiuka amri hiyo kuwa atafikishwa mahakamani.

Sehemu ya mlima liyochomwa moto na mtu asiyejulikana, Picha na Adelinus Banenwa

Mkuu huyo wa wilaya  pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya usalama ya wilaya wameshiriki kuzima moto ambao ulikuwa ukiwaka kwenye moja ya mlima unaozunguka ofisi ya mkuu wa wilaya huku aliyewasha moto huo kutotambulika.

Sauti ya DC Dkt Vicent Naano