Mazingira FM

“Serikali ikemee ukiukwaji wa maadili, mila na utamaduni wetu”

14 June 2024, 5:05 pm

Kongamano la wazee kuelekea siku ya kupinga ukatili dhidi ya wazee June 15 Bunda,Picha na Adelinus Banenwa

Sisi kama wazee tutatoa tamko la suala la maadili haya kupinga ndoa za jinsia moja na ulawiti hapa nchini”

Na Adelinus Banenwa

Wazee wameiomba serikali kukemea matendo ya ukiukwaji wa maadili, mila na desturi kwenye jamii hasa kizazi cha sasa.

Hayo yamesemwa kwenye kongamano la wazee ikiwa ni siku ya pili kuelekea maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili dhidi ya wazee.

Kongamano la wazee kuelekea siku ya kupinga ukatili dhidi ya wazee June 15 Bunda,Picha na Adelinus Banenwa.

Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa chuo cha ualimu Bunda na kuwakutanisha wazee mbalimbali kutoka kila kona ya Tanzania ambapo mgeni rasmi akiwa mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mara Kanal Evans Mtambi.

Katika kongamano hilo wazee mbali na changamoto zingine wameelezea suala ushirikishwa wa mambo kwenye jamii, suala la ukosefu wa matibabu ya uhakika, kutelekezwa na watoto bado ni kikwazo kwao Aidha wametaja suala malezi kuzingatiwa hasa matendo ya ndoa za jinsia moja, ulawiti,ubakaji viendelee kukemewa kwenye jamii.

Joseph Mbasha meneja program kutoka shirika la HelpAge Tanzania, Picha na Adelinus Banenwa

Kwa upande wake Joseph Mbasha meneja program kutoka shirika la HelpAge Tanzania amesema wao kama taasisi ambayo inafanya kazi kwa karibu katika kusaidia mambo yanayohusu wazee wanaziona changamoto baadhi kama vile suala la matibabu kwa wazee, kushirikishwa na kutelekezwa.

Mbasha ameongeza kuwa taasisi ya HelpAge inafanya kazi kwa karibu na halmashauri na wizara ambao zihusika na utetezi wa makundi maalumu kama vile wizara ya Maendeleo ya jamii ili kwa pamoja kuzitatua changamoto za wazee.