Vijana watakiwa kujitambua na kuachana na tabia zisizofaa
2 June 2024, 3:39 pm
Vijana watakiwa kujitambua na kuachana na tabia zisizofaa kwa kuwa wao ndiyo nguzo ya familia na jamii
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa vijana kujitambua kuwa wao ndiyo nguvu ya familia na jamii hivyo hawana budi kuachana na makundi yasiyofaa kwenye jamii kama vile uvutaji wa bangi.
Wito huo umetolewa na mchungaji Jeremiah Motomoto mchungaji kiongozi kanisa la Buptist Nyasura kwenye tamasha la vijana wa makanisa ya Buptist ambalo limefanyika tarehe June 1, 2024 kwenye kanisa la Buptis Nyasura .
Tamasha hilo lililowakutanisha vijana zaidi ya 600 limetajwa kuwa linalenga kutumia vipawa na karama za vijana katika kumtumikia mungu kupitia uimbaji na vipaji vingine.
Akizungumza na Mazingira Fm muandaaji wa tamasha hilo Elisha Motomoto ameseama matarajio yao kama kanisa ni kuona taifa linakuwa navijana wenye kumcha na kumtumikia Mungu.
Nao vijana waliofika kwenye tamasha hilo wamesema ni matarajio yao kuona kizazi hiki kinamtumikia Mungu kupitia karama ya uimbaji na vijana hasa ndiyo walengwa
Kwa upande wake wake mchungaji Jeremiah Motomoto mchungaji kiongozi kanisa la Buptist Nyasura amesema mbali na vijana kutumia tamasha hilo kwa ajili ya kuonesha karama za uimbaji pia kuna mafundisho kwa vijana namna ya kumuishi Mungu, kutunza na kutimiza ndoto zao katika ulimwengu wa utandawazi.