Mazingira FM

Million 15 zatengeneza madawati Bunda mjini

30 May 2024, 2:01 pm

Katibu wa mbunge wa jimbo la Bunda mjini Emmanuel Kija, Picha na Adelinus Banenwa

Fedha za mfuko wa jimbo la Bunda mjini ni kiasi cha shilingi milioni 58.7 za mwaka 2023 na 2024 zimetumika kwa kiasi kikubwa kutengeneza madawati.

na Adelinus Banenwa

Zaidi ya million 15 za mfuko wa jimbo mwaka 2023 na 2024 zatumika kutengeneza madawati jimbo la Bunda Mjini.

Hayo yamebainishwa na Katibu wa mbunge wa jimbo la Bunda mjini Emmanuel Kija kwa niaba ya mbunge Mhe Robert Chacha Maboto mapema leo kwenye kipindi cha Asubuhi leo kupitia studio za radio Mazingira Fm.

Emmanuel amesema mbali na milioni 15 kutengeneza madawati pia fedha nyingine imetumika katika kuunga juhudi za wananchi katika ukamilishaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo kama vile Zahanati, ofisi za serikali za mitaa n.k

Katibu wa mbunge wa jimbo la Bunda mjini Emmanuel Kija, Picha na Adelinus Banenwa
Sauti ya Emmanuel Kija

Aidha Katibu huyo amesema pamoja na fedha za mfuko wa jimbo kufanya kazi hizo pia mhe mbunge anaendelea na adhma yake ya kutumia mshahala wake kuwahudumia wananchi ambapo kila mwezi anatumia shilingi milion 2 hadi 3 kulipia gharama za matibabu kwa wakazi wa jimbo la Bunda mjini wasiyokuwa na uwezo wanaofika hospitali ya Bunda DDH kupata matibabu.

Sauti ya Emmanuel Kija

Katibu huyo amesema fedha hizo za mfuko wa jimbo la Bunda mjini ni kiasi cha shilingi milioni 58.7 za mwaka 2023 na 2024.