Mbunge Agness Marwa ampongeza Rais Samia kwa miradi ya maendeleo Bunda
29 May 2024, 6:37 pm
Tuna kila sababu ya kumshukuru Rais Dr Samia kwa kuleta fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa wananchi wilayani Bunda hasa kata ya Bunda stoo
Na Adelinus Banenwa
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara mhe Agness Mathew Marwa amempongeza Rais Samia Suluhu Hasani kwa kuleta miradi mingi ya maendeleo kwa wananchi wilayani Bunda.
Mhe Agness ameyasema hayo mara baada ya ziara yake kwenye kata ya Bunda stoo ambapo amekagua miradi ya ujenzi wa hospitali ya halmashauri ya mji wa Bunda pamoja shule ya msingi ya Bunda stoo iliyojengwa kwa mradi wa BOOST.
Mhe Agness amesema inatia moyo sana kuona zaidi ya shilingi bilion 2.3 hadi sasa kwenye hospitali na milioni 540 ujenzi wa shule ya msingi zinatolewa na serikali ili wananchi wapate huduma.
Kwa upande wake diwani wa Bunda stoo Flaviani Chacha amesema mbali na mafanikio mengi changamoto kubwa kwa kata ya Bunda stoo ni suala upungufu wa mtandao wa maji kutoka mamlaka ya maji Bunda pia barabara za kata zina hali mbaya kutokana na kuharibiwa na mvua.