Mazingira FM

“Ukosefu wa chakula shuleni chanzoa wanafunzi kufanya vibaya kitaaluma”

29 May 2024, 6:25 pm

Mwalimu James Elias Chisanga kutoka ofisi ya mdhibiti ubora wa elimu halmashauri ya wilaya ya Bunda, Picha na Adelinus Banenwa

Imetajwa kuwa chakula shuleni ni muhimu ili kuongeza hali ya mwanafunzi kufanya vizuri kitaaluma.

Na Adelinus Banenwa

Suala la ukosefu wa chakula mashuleni, walimu kutotimiza majukumu yao pamoja na ushilikiano kati ya wazazi na walimu imetajwa kama chanzo cha kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi halmashauri ya wilaya ya Bunda.

Hayo yamesemamwa na ofisi ya mdhibiti ubora wa elimu halmashauri ya wilaya ya Bunda pamoja na waheshimiwa madiwani kwenye kikao cha baraza la madiwani cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2023 na 2024.

Sauti ya Mwalimu James Elias Chisanga

Katika hoja zao waheshimiwa madiwani wamesema changamoto ya wanafunzi kukosa chakula ambapo wazazi wengi hawachangii vyakula hivyo kusababisha ufaulu kushuka pia wameitaka ofisi ya mdhibiti ubora wa elimu kuhakikisha wanawafutilia walimu ili waweze kufanya kazi kwa weledi ili wawe wanamaliza mitaala.

Moja ya madiwani akichangia kuhusu umuhimu wa wanafunzi kupata chakula mashuleni

Kwa upande wake Mwalimu James Elias Chisanga kutoka ofisi ya mdhibiti ubora wa elimu halmashauri ya wilaya ya Bunda amesema ufaulu wa wanafunzi unachangiwa na mambo mengi ikiwemo kutokuwepo ushilikiano baina ya wazazi na walimu, ukosefu wa chakula mashuleni miongoni mwa sababu zingine.

Naye mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano amewaagiza madiwani kushawishi na kusimamia wazazi na walezi kuchangia chakula mashuleni ili kuwafanya wanafunzi wajifunze kwa ufanisi.

Sauti ya DC Naano