Mazingira FM

Aliyepatwa na ugonjwa wa ajabu, amuomba Rais Samia na wadau kumsaidia matibabu

19 May 2024, 2:28 pm

Arnold Eflon miaka 21 aliyepatwa na ugonjwa wa ajabu, Picha na Adelinus Banenwa

Alianza kwa kutokwa na damu puani mwaka 2021 akiwa kidato cha nne ikafuatiwa nyama za puani, amefanyiwa upasuaji mara mbili hospitali ya Bugando.

Na Adelinus Banenwa

Arnold Eflon miaka 21 aliyepatwa na ugonjwa wa ajabu amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumsaidia matibabu ili aendelee na masomo yake.

Kijana Arnold ni mwenyeji wa wilaya ya  Buchosa mkoani Mwanza ambapo kwa sasa anaishi kijiji cha Makwa kata ya Nampindi wilayani Bunda akiwa na baba yake mzazi.

Arnold Eflon miaka 21 aliyepatwa na ugonjwa wa ajabu akiwa na baba yake mzazi Eflon Masumbuko Tutuba , Picha na Adelinus Banenwa

Eflon Masumbuko Tutuba baba mazazi wa Arnold anasema tatizo la mwanae lilianza tangu mwaka 2021 akiwa kidato cha nne alianza kutokwa na damu puani kisha vikaanza kuota vinyama puani ambapo amefanyiwa upasuaji mara mbili hospitali ya Bugando.

Masumbuko amesema Arnold alifaulu mtihani wa kidado cha nne kwenda chuo lakini imeshindikana kutokana na hali yake pia kutumia fedha nyingi katika matibabu ya mwanae ambapo alilazimika kuuza mali zake zote ikiwa ni mifugo pamoja na mashamba  ili kusaidia matibabu.

Arnold Eflon miaka 21 aliyepatwa na ugonjwa wa ajabu akiwa na baba yake mzazi Eflon Masumbuko Tutuba , Picha na Adelinus Banenwa

Masumbuko amemuomba Rais Samia, serikali pamoja na wadau wote kumsaidia mwanae apate matibabu ili aendelee na masomo yake maana kwa sasa yeye hana tena cha kumsaidia kutokana na kuishiwa rasilimali zote.

Eflon Masumbuko Tutuba, baba mzazi wa Arnold Eflon

Kwa upande wake Arnold anasema ugonjwa huu unamsumbua sana hasa wakati wa usiku kichwa kinamuuma sana pia anapumua kwa shida, ameomba msaada wa matibu kwa Rais Samia ili aweze kupona na kuendelea na masomo yake.