Mazingira FM

Tukosawa wahimiza utunzaji mazingira Bunda

19 April 2024, 4:47 pm

Madaraka Nyerere ambaye ni balozi wa mtandao wa Tukosawa , Picha na Avelina Sulusi

Madaraka Nyerere atembelea shule yenye jina la Nyerere awataka wanafunzi kutunza mazingira awahaidi kuwakaribisha Butiama.

Na Avelina Sulusi

Wito umetolewa  kwa Jamii kutunza  mazingira   na kuyashika mafunzo katika utunzaji wa mazingira ili iwe faidi kwao kwa baadaye

Hayo yamesemwa na Madaraka Nyerere ambaye ni balozi wa mtandao wa Tukosawa  alipotembelea shule ya msingi Nyerere ilayopo Bunda mjini ambapo amealikwa kama mgeni rasmi katika kikao cha Tukosawa ambao mtandao huo unajishughulisha na masuala ya utunzaji wa mazingira.

Madaraka Nyerere ambaye ni balozi wa mtandao wa Tukosawa , Picha na Avelina Sulusi

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyerere Edwin Johakimu Byangwamu amesema mtandao wa tukosawa unaamini juu ya utu, upendo na umoja ambayo dhana yake kuu ni kwaajili ya kizazi cha sasa na kijacho katika kutunza mazingira.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyerere Edwin Johakimu Byangwamu, Picha na Avelina Sulusi

Byangwamu amesema jumuiya ya tukosawa katika kutunza mazingira inaamini vitu vyote vilivyoumbwa katika dunia hii viko sawa na vinapaswa kutunzwa na kuendelezwa, amabapo amesema shughuli zilizofanywa na tuko sawa ni pamoja na  kupanda miti ya matunda, vivuli, mbao , mbogamboga  ambazo hutumiwa na wanafunzi na jamii nzima inayowazunguka.

Akisoma  taarifa fupi  juu ya changamoto wanazokutana nazo katika kutekeleza kazi za kikundi cha Green Rubana Women Group  Bi Rose Costantine ambaye ni katibu wa kikundi hicho amesema anaomba kikundi chao kupata mafunzo na uzoefu kutoka vikundi vingine juu ya utunzaji wa mazingira.

 Aidha ameiomba ofisi ya   tukosawa kuweza kuendeleza ushirikiano ili shughuli za kikundi ziweze kuwapatia mbinu mbalimbali za ufanisi katika shughuli zao kwani shughuli zao zinategemea nguvu zao wenyewe.