Jumuiya ya wazazi CCM Bunda yalaani tukio la mwanafunzi kubakwa, kulawitiwa
15 March 2024, 4:25 pm
Jumuiya ya wazazi CCM Bunda yalaani mwanafunzi kubakwa, kulawitiwa yaitaka serikali kubitia vyombo vyake kuhakikisha sheria inachukue mkondo wake kwa atakayethibitika kutenda kosa hilo.
Na Adelinus Banenwa
Mwenyekiti wa wazazi CCM wilaya ya Bunda wakili Leonard Magwayega amekemea vikali kitendo cha mwanafunzi wa darasa la Sita (16)( jina linahifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya watoto ya mwaka 2009) kubakwa na kulawitiwa na mtu anayetajwa kuwa ni mwalimu wake mkuu.
Wakili Magwayega amesema tukio la kikatili alilofanyiwa mwanafunzi huyo halikubaliki kijamii na kisheria na anaiomba serikali kupitia wataalamu wake kufanya uchunguzi kwa mtuhumiwa ili ikibainika kuwa ni yeye amefanya hivyo hatua za kisheria zichukuliwe
Aidha amesema walimu wamepewa dhamana kubwa ya malezi kwa watoto hivyo kusikika mwalimu anatuhumiwa kutenda tukio hilo inasikitisha japo hawawezi kuhukumu moja kwa moja maana chombo pekee chenye kuthibitisha hilo ni mahakama pekee kwa mujibu wa sheria za nchi.
Wakili Magwayega ameyasema hayo jana 14/3/2024 katika kikao alichokifanya na viongozi wa chama, serikali, kamati ya shule ya msingi ya Masaunga pamoja na walimu alipokuwa anasoma mwanafunzi huyo huku akiwa ameambatana na Katibu wa jumuiya ya wazaziCCM Bunda Lucia John Tabuse, Katibu Elimu, Malezi na Mazingira, Ndg Masau na Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Wazazi Wilaya Ndg Hidaya Juma,